Mnamo Februari tarehe 27 (Jumanne), 28 (Jumatano), na 29 (Alhamisi) mwaka huu wa 2024 tutakuwa na Kambi Ya Macho pale wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma katika Hospitali ya Halmashauri ya Kondoa iliyopo Bukulu tukitoa Huduma Ya Macho BURE kabisa, kuanzia saa 2 asubuhi.
Mawasiliano Kondoa: 0787 253 427 au 0713 253 417.
Tunakukaribisha uje, pamoja na ndugu jamaa na marafiki kuchunguza macho na kupata matibabu BURE!
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kwenye Kambi ya Macho
1.) Je, mna vigezo vyovyote ili kupata huduma?
Hapana. Mtu yeyote anaruhusiwa kuja kupata huduma.
2.) Ninahitaji kupiga simu kabla ya kuja?
Hapana. Unaweza kuja wakati wowote kuanzia saa 2 asubuhi, tarehe 27, 28, 29 Februari pale hospitali ya Halmashauri iliyopo Bukulu, Kondoa. Ukifika utahudumiwa!
3.) Nitahitaji kulipia ile nitibiwe?
Hapana. Ni BURE kabisa.
4.) Ni huduma gani nitazipata kwenye kambi ya macho?
- Kupima macho, bure!
- Dawa za macho, bure!
- Miwani ya kusomea, bure!
- Hudma ya upasuaji wa mtoto wa jicho, bure!
- Watakaolazwa baada ya upasuaji watapewa chakula, bure!
5.) Je, ninaweza kuja na familia yangu?
NDIYO! Tunashauri uje na wazazi, babu, bibi na wote watanufaika ni huduma ya macho.
6.) Nitapewa miwani nikihitaji?
Daktari akishauri upate miwani basi utapata miwani bure!
Tufwate kwenye mitandao yetu ya Jamii kwa taarifa zaidi. Bofya hizi tovuti na upelekwe kwenye kurasa zetu moja kwa moja: